Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla kushiriki katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana mwaka 2016, yatakayofanyika mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yatakayofanyika Oktoba 14, 2016 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mtaka ameeleza kuwa Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia atashiriki Ibada ya Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, itakayofanyika siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana, Mjini Bariadi kuanzia saa 1:00 kamili asubuhi.

Wakati huo huo Mtaka amesema maadhimisho ya wiki ya vijana yatafunguliwa rasmi tarehe 08 Oktoba, 2016 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) katika Uwanja wa SABASABA Mjini Bariadi; ambapo shughuli mbalimbali za vikundi vya maendeleo ya vijana kutoka Halmashauri zote nchini zikiwemo za ujasiriamali pamoja na ugunduzi wa kisayansi ambao umethibitishwa na Tume ya Taifa ya Sayansi zitaoneshwa katika mabanda maalum yaliyojengwa katika uwanja huo.

“Kwa upande mkoa wa Simiyu vikundi vyetu vya vijana vimejiandaa kuonesha shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanywa katika Halmashauri husika;ambapo kimkoa tunatekeleza mkakati wa kila wilaya kuzalisha bidhaa/huduma moja yaani (one district one product). 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Oktoba 14 mwaka 2016, yatakayofanyika mkoani humo. 
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Maswa wakiwa katika zoezi la uzalishaji chaki katika kiwanda cha kutengeneza chaki kilichopo wilayani humo ambacho kinazalisha chaki zinazotambulika sokoni kama Mzinazotumika mkoani Simiyu.
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Meatu wakielekezwa namna ya kupima maziwa na kutambua maziwa bora yasiyo na maji, katika kiwanda chao cha uzalishaji wa maziwa yanayotambulika sokoni kama ‘MEATU MILK’.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...