NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

WANANCHI wa kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni  wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli kuingilia kati haraka iwezekanavyo migogoro  ya kugombania  ardhi baina ya wafugaji na wakulima ya  ili kuweza kuepeukana  vurugu na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kusababisha baadhi ya watu kupoteza maisha yao na uvunjifu wa amani.

Kilio hicho wamekitoa kwa mbunge wa jimbo la Rufiji wakati wa mkutano wa adhara  katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni  ulioandaliwa  kwa lengo la kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabii wananchi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

 Wanakijiji hao akiwemo Juma Katoto na  Salum Mlanzi walisema kwamba kulingana na kukithiri kwa mapigano ya wakulima na wafugaji serikali inapaswa kulitafutua ufumbuzi suala hilo kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kufanya utaratibu wa kuipunguza mifugo iliyozidi kwani ndio chanzo cha kusababisha vurugu hizo.

Aidha katika hatua nyingne walisema  kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika mashamba na kula mazao yao hali ambayo  kwa sasa imesababisha kuwepo kwa njaa katika baadhi ya maeneo kutokana  na kukosa chakula .

“Kwa kweli kwa sasa sisi wananchi wa kijiji hiki cha mloko bado tunakabiliwa na changamoto ya wakulima na wafugaji, maana tatio kubwa ni jamii ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba yaetu na kua mazao yote kama vile, mahindi, mpunga, mboga mboga amabo ndizo tunategemea katika chakula, hivyo serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali a kisheria,”alisema wananchi hao.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la rufiji Mohamed Mchengerwa ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa kushirikiana  bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano  katika  kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu   kwa ajili ya wagugaji na wakulima ili kuepukana na  mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa wananchi wake.

Mchengerwa aliesma kwamba anatambua kuwepo kwa changamoto hiyo ya wafugai kuingiza migugo kiholela katika maeneo ya mashamba, lakini ameshaana kufanua jitihada  hali na mali kuhakikisha kuwa serikali inatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wakulima na wafigaji ili kuweza kuondokana na virugu amabo imekuwa ikijitokeza.

“Katika jimbo langu la rufiji kwa sasa kuna zaidi ya mifugo kama laki tatu na nusu hadi laki nne kwa hivyo kikubwa aidi hapa mii nitahakikisha kwamba vurugu hizi zinamalizika kwa kushirikiana  na serikali ili kuweza kuona jinsi ya kutoa elimu kwa jamii ya wafugaji na wakulima ,ii wananachi wawee kuishi kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano ya aina yoyote,”alisema Mchengerwa.

WILAYA  ya rufiji kwa sasa ambayo inakadiriwa kuwa na mifugo zaidi ya laki tatu na nusu  bado inakabiliwa na changamoto  ya migogoro ya ardhi kwa kipindi cha muda mrefu kutokana  na jamii ya wakulima kuamua kuingiza mifugo yao katika maeneo ya mashamba na kula mazao hali ambayo inasababisha kuibuka kwa matukio ya mapigano na uvunjifu wa amani .
 Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara kwa lengo la kuweza kujadili changamoto mbali mbali inazowakabili
 Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwahutubia wananchiwa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha mloka wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengwerwa wakati  wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mloka.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa


  1. Kila kitu Mheshimiwa Magufuli atatue, je viongozi wahusika wako wapi? Na wabunge wahusika pia wako wapi? Wabunge wa majimbo yenye migogoro bila suluhisho kwa miaka mingi pamoja na mawaziri husika na viongozi wa serikari maeneo hayo - Mkuu wa Mkoa na Wilaya watumbuliwe wote kwa kutokiwa-effective
    Mdau Josheffu, dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...