Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii 

SERIKALI imetoa miezi mitatu kwa watu wanaomiliki viwanja kwa ofa ya jiji ili kuweza kupata hati baada ya kubainika kuwepo kwa matapeli wa kugushi nyaraka za serikali kwa  viwanja hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesesema katika uhakiki huo wameweza kubaini  Raia mwenye asili ya Asia, Hamant Patel kumiliki ardhi kwa viwanja vitano katika mikoa mitatu.
Amesema kuwa waliopewa viwanja kwa ofa ya jiji, hati hizo zitatolewa na Kamishina wa ardhi na watakaobainika kugushi nyaraka hizo watafikishwa katika vyombo vya dola kutokana na kuibuka kwa migogoro katika viwanja hivyo.

Waziri, Lukuvi amesema kuwa watu wenye uraia wa nje na si watanzania hawana uwezo kupata ardhi nchini na wanachotakiwa kufanya ni kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) ndio wanaweza kutoa ardhi.

Amesema kuna baadhi ya wawekezaji wamekuwa wakiwaweka watanzania katika hisa na baada ya kufanikisha jambo lao la kupata ardhi wanahisa watanzania wanajitoa. Aidha amesema kuwa kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye kilichokuwepo Mabwepande kimefutwa umiliki kutokana na kushindwa kuendelezwa kwa muda na baadae kuvamiwa na wananchi.

Amesema serikali haitaangalia mtu usoni kwa watu kumiliki ardhi bila kuendeleza kwa muda mrefu huku kukiwa na viwanja vingine kukosa mapato yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...