Na Lorietha Laurence-WHUSM 

Wasanii wa Muziki wa Singeli wameaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali yatakayowasaidia kuongeza weledi na mbinu za kukuza kazi zao na hatimaye kuwa na sanaa bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam. 

Bi Joyce aliongeza kwa kusema kuwa sanaa ya muziki ni kazi kama kazi nyingine hivyo ni budi kusimamia misingi iliyo bora inayoendana na utamaduni wa kitanzania katika utunzi wa tungo za singeli. 

“Utamaduni ni mali ya jamii hivyo ni jukumu letu sote kupenda,kuthamini na kuendeleza utamaduni wetu kupitia kazi za sanaa na hii itasaidia kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni” alisema Bi.Joyce. 

Aidha aliupongeza uongozi wa EFM kwa kuandaa semina hiyo ambayo imewapa fursa wasanii kupata elimu ya msingi kuhusu muziki na kuifanya kazi ya sanaa kuwa ya thamani kwa jamii. 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mkuu wa EFM Bw.Denis Ssebo na kushoto ni Mkurugenzi wa EFM Bw. Francis Ciza. 
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi akiwasisitiza wasanii (hawapo katika picha) matumizi sahii ya mitandao ya kijamii wakati wa semina ya wanamuziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam.  
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu(wa tano kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa muziki wa singeli baada ya semina iliyokuwa imeandaliwa na uongozi wa Radio EFM jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...