Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchinii ,wanatarajia kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) leo (jana) wameingia Rasmi mkoani Arusha na kutembelea ofisi za gazeti la The Guardian na Nipashe ikiwa ni moja ya kazi ambazo watazifanya wakiwa mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapa leo (jana) na wanakaa kwa muda wa siku tatu ,na katika siku hizo wanampango wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.Aidha alisema kuwa pia ndani ya siku hizo tatu kutakuwepo na shindano la Top model ambalo litafanyika Jumamosi October 15 katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha 

"tunafanya shindano hilo katika ukumbi wa triple A, natunarajia wananchi wengi wa Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo ni shilingi 10,000 tu, hivyo napenda kutumia mda huu kuwaalika wananchi wa Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa Top Model"alisema Makoye 

Alisema kuwa mbali na hapa warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma,Singinda ,Dar es Salaam hapa Arusha na hatimaye wanatarajia kuondoka na kwenda Mwanza ambapo ndipo shindano hili linafayanyika kwa mwaka huu .

Alisema kuwa shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika october 29 katika ukumbi wa Rock City Mall ambapo alibainisha hadi sasa warembo wote 30 wapo vizuri na wanasubiria siku yenyewe ifike na maandalizi ya shindano yamekamilika

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha The Gardian /Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara Edward Qorro alitoa shukrani kwa warembo hao kuwatambelea na kuwatakia kila la kheri katika mashandano hayo wanayotarajia kushiriki hivi karibuni.

Warembo 30 wanaoshiriki kinyanganyiro cha kumsala Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara tu baada ya kutembelea ofisi za gazeti la Guardian zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha 
picha ikionyesha baadhi ya warembo akiwemo mwenyeji wao ambaye ni miss Arusha wa pili kulia Maurine Ayubu wakiwa ndani ya ofisi za gazeti la Gurdian na Nipashe zilizopo jiji Arusha
Msimamizi wa kituo cha Gazeti la Gurdian na Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara Edward Qorro akiwa anatoa maelekezo mafupi kwa warembo juu ya kazi zinazofanya na magazeti hayo katika mkoa huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...