THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANTRADE YAENDESHA MAFUNZO YA USHONAJI NGUO WATU WASIOONA


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeanzisha mafunzo ya Ushonaji Nguoa kwa watu wasioona ambayo yatatolewa kwa miezi mitatu kuendeshwa na fundi mahiri wa nguo za kushona, Abdallah Nyangalio.

Akizungumza na katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia watu wasioona kuweza kujiajiri na kuongeza kipato cha kuacha kuombaomba.

Amesema kuwa mwanafunzi mmoja ambaye atafanya vizuri katika mtihani wa mafunzo hayo atatoa cherehani ikiwa ni pamoja na mwanafunzi mmoja wa Temeke kwa kila mzunguko atatoa cherehani moja.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Edwin Rutageruka amesema kuwa kuendesha mafunzo hayo ni kutaka watu wasioona waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa mafunzo ya ushonaji nguo.

Rutageruka amesema kuwa Mamlaka imeona kendesha mafunzo katika wilaya tano kwa kuanzia kwa Manispaa ya Temeke kwa kila Darasa litakuwa na watu saba.Mkufunzi wa mafunzo hayo, Abdallah Nyangalio amesema kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya kila kitu na kuwa hivyo sio kigezo cha kufanya kuombaomba.
Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva (kulia) akimkabidhi zawadi ya Cherehani Mkufunzi wa Mafunzo wa ushonaji kwa wasioona Bw. Abdallah Nyangalio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam,wa kwanza kusoto ni Bw. Edwin Rutageruka Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Picha na Benjamin Sawe Maelezo).
Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva (kulia) akiongea na Mkufunzi wa Mafunzo wa ushonaji kwa wasioona Bw. Abdallah Nyangalio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa wilaya hiyo amewaasa watu wenye ulemavu kutokata tamaa kimaisha kwani jambo lolote ukiwa na nia nalo na kulifanya kwa nidhamu na kujituma utafanikiwa(Picha na Benjamin Sawe Maelezo).