THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WATANZANIA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI.

Na. Eliphace Marwa – Maelezo 

Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania kuongeza thamani ya bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.

Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan (JICA).

“Tuko hapa hii leo kushuhudia sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya viwanda ambayo ni matunda ya dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili kuweza kutoa changamoto kwa makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase aliipongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa sherehe yenye mafanikio kwa mara nyingine kufuatia ili iliyofanyika mwaka jana.

“Baada ya uzinduzi wa mpango wa miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa kukuza viwanda ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa Tanzania”, alisema Bw. Toshio

Aidha Bw. Toshio alibainisha baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na kutoa motisha kwa wafanyakazi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema kuwa anaamini kuitangaza KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili kutengeneza viwanda vyenye ushindani na kufanikisha lengo la kukuza viwanda kuelekea mwaka 2025.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu toka kushoto waliokaa) pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi wa JICA Tanzania wakiwa katia picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo