“Tukiwa tunasherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2016,tunajivunia kuwa sehemu ya maendeleo na mafanikio yako ya Familia yako,tunaahidi kukupatia suluhisho la masuala ya kibenki ambayo si tu kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zako, lakini pia kukuhamasisha wewe kufanikiwa zaidi,”ilisema taarifa hiyo.

CRDB  iliwashukuru wateja kwa kuichagua Benki ya CRDB na kwamba matumaini yao ni kuendelea kufurahia huduma zao  ambazo  ni za kibunifu.

“Kwa unyenyekevu  na furaha kubwa,kwa niaba ya familia ya Benki ya CRDB nachukua fursa hii kukushukuru kwa kuendelea kutumia huduma zetu, sisi kama Benki tunaamini kwa kiasi kikubwa katika kujenga mahusiano ya kudumu na wateja wetu, siku zote tutaendelea kushirikiana nawe katika kutimiza malengo yako na kufurahia mafanikio tunayopata kwa pamoja".
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akizungumza na Wateja pamoja na Wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni muendelezo wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 3 Duniani kote ambapo wateja wa CRDB wataendelea kujivunia  mafanikio ya Benki hiyo.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Mohamed Madengelo akizungumza na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Sherehe hiyo ilipambwa kwa keki.


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akishirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Easy Connections, Justus Bashara wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...