Kwa
mara ya kwanza nchini Tanzania, Kampuni ya SS Brand International
imeandaa Maonyesho ya Watoto yenye lengo kuhamasisha na kutangaza
bidhaa, huduma na miradi ya watoto ili kukuza na kutoa upendeleo
unaohitajika kuweza kuhamasisha utumiaji wa bidhaa bora za watoto.
Akizungumza
katika kilele cha tamasha hilo la siku tatu lililofanyika katika Ukumbi
wa Mlimani city jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa SS Brand
International, Batul Adam amesema, tamasha hilo liliweza kuvutia watu
mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali za watoto,
wanahabari na familia ambao waliweza kujipatia taarifa kuhusu bidhaa na
huduma za watoto zinazotolewa na makampuni hayo.
Huduma
mbalimbali ziliweza kupatikana ikiwamo huduma ya bima ya Afya ya mtoto
kutoka NHIF yaani Toto Afya, huduma za upimaji wa macho bure uliofanywa
na kampuni ya Internatioal Eye Hospital, huduma zingine za bima kwa
watoto, bidhaa za watoto na wakubwa na bidhaa nyingine, maelezo ya afya
kutoka kwa wataalam n.k
Watoto
wadogo waliopelekwa na wazazi wao katika maonyesho hayo, waliweza
kushiriki mashindano ya kutambaa kwa wale wa kati ya umri wa kuanzia
miezi mitano mpaka kumi na mbili ambayo yalidhaminiwa na bidhaa ya
Softcare ya Sunda International na mshindi kujipatia diapers za kutumia
miezi sita.
Maonyesho hayo yalidhaminiwa na kampuni ya Dar Fresh na Afiya, NHIF, Sundal International, PEPSI, MITAN.
Mashindano
hayo yanategemea kufanyika tena baada ya miezi sita ambapo inatarajiwa
makampuni mengi zaidi yataweza kushiriki na kuweza kutoa huduma na
taarifa kuhusu bidhaa zao ipasavyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa SS Brand Internnational, Batul Adam akizungumza na
Michuzi Tv kuhusu tamasha la maonyesho ya watoto katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Watoto waliofika kwenye tamasha hilo wakecheza michezo mbalimbali leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wazazi na walezi waliowate Watoto kwenye tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...