Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe Augustine Mahiga yupo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 13 Oktoba, 2016.

Mhe. Mahiga ambaye anaongoza ujumbe wa Mawaziri wa Asasi hiyo yupo nchini humo kwa maagizo ya Mwenyekiti wa Asasi, Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kutathmini hali ya siasa ilivyo nchini humo ili kushauri ipasavyo.

Aidha, tathmini hiyo inafanyika kufuatia hali tete ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama nchini DRC iliyochangiwa na maandamano yaliyofanyika tarehe 19 Septemba, 2016 ambayo yaliandaliwa na vyama vya upinzani kwa lengo la kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya DRC (CENI) kutangaza tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. 
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa sita kushoto) akiongoza kikao cha pamoja cha Mawaziri kilichofanyika katika Hoteli ya Pullman, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wengine katika picha upande wa kulia ni Mabalozi wa Nchi wanachama wa SADC wanaowakilisha nchi zao DRC. 
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiongoza ujumbe wa SADC katika kikao alichokifanya na Mhe. Raymond Tshibanda (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC ambaye aliongozana na viongozi wa juu wanaoratibu uchaguzi nchini DRC. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...