Na Stella Kalinga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kusindika maziwa kinachoendeshwa na kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani humo Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na Vijana hao wanaosindika maziwa ya Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na Serikali kwa ujumla. 

Mhagama amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika la maziwa.

Aidha, Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka za kuwatengenezea vijana mazingira mazuri ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Wakati huo huo Waziri Mhagama ameahidi kuwa Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi 30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kuongeza uzalishaji ili kupanua soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kabla ya kuzindua kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akipewa maelezo na vijana wa kikundi cha Meatu Milk wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa kabla ya kuweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa Meatu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...