Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo akiongea na baadhi ya Wananchi ambao Nyumba zao ziliathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiandana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44 na kusababisha madhara makubwa
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Vijijini akikagua baadhi ya nyumba zilizoathirika na upepo mkali katika kijiji cha Kiembe Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 usiku upepo mkali ukiandamana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo na Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini akiwa amekaa kwenye moja ya nyumba akikagua baadhi ya Nyumba zilizoathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. 

Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiendana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44. Nyumba Nyingi zilizoathirika ni zile za mgongo wa Tembo. Katika kukagua athari za uharibifu ilibainika myumba Tano ziliathirika vibaya kiasi cha kusababisha wamiliki wake kulala Nje.

Hata, hivyo ilielezwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Viongozi wa Halmashauri walitembelea eneo hilo baada ya kupata taarifa za athari za kuezuliwa paa na kuahidi kuagiza tathmini ifanyike ili Serikali iweze kutoa masaada kwa Wananchi hao.

kuongea na Wananchi hao, Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijini aliiwaambia Wananchi hao kuwa Serikali ya Rais Magufuli ipo pamoja nao na ametumwa kuwapa pole kutoka kwa Viongozi wa juu wa Serikali. "Ndugu wananchi, nimetumwa na Rais wetu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli niwape pole sana kwa kukutwa na kadhia hii ya kuenguliwa Nyumba Zenu na upepo, aidha, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanawapa pole pia na wanawatakia heri wale wote walioathirika"

Prof. Muhongo aliwaelekeza Viongozi wa kijiji hicho kuwa wahakikishe wanafanya tathmini ya kweli kwa kupita kila Nyumba iliyoathirika na yoyote atakaegundulika Amedanganya ili alipwe zoezi zima litaahirishwa na kurudiwa upya, pia wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, aliwaahidi Wananchi hao kuanza kupewa misaada Baada ya kikao Cha Halmashauri kupitia taarifa ya tathmini jumatatu tarehe 17/10/2016 na kuwaelekeza Viongozi wa Halmashauri kufanya kazi hiyo kwa haraka.

Prof. Muhongo alikuwa Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya kukagua umeme Sambamba na kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere iliyofanyika nyumbani kwake Butiama tarehe 14/10/2016

HABARI PICHA KWA HISANI YA ANNA NKINDA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tuanze mchango mwingine tena!!!'m

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...