NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

SERIKALI imewaagiza wakuu wa Mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wote nchini kuweka programu kwa ajili ya kutenga maeneo maalumu yatakayotumika kwa ajili ya uwekezaji wa kujenga viwanda lengo la kuweza kuwakomboa vijana kupata soko la ajira ambalo litaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 9 ya wajasiriamali mbali mbali kutoka mikoa mitano ya kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.

Mwijage alisema kwamba mikakati ya serikali ya awamu ya nne ni kuwa na nchi yenye viwanda vya aina mbali mbali ambavyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wimbi la umasikini na kuwataka watendaji na viongozi kuchana na tabia ya kuuza maeneo kiholela.

Aidha Mwijage alibainisha kwamba shirika la viwango Tanazania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na TFDA kuhakikisha wanapunguza tozo za viwango na kutokwamisha vibali kwa wafanyabiashara wado wadogo na badala yake wawapatia fursa ya kuweza kuuza bidhaa zao kwa urahisi bila ya kuwa na masharti mengi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO) Tanzania Profesa Syvester Mpanduji amesema kuwa kwa sasa wameshafanya maonyesha ya kitaifa 97 ya wajasiriamali ambayo yameweza kuwaingizia kiasi cha shilingi billion 16.8,na kuongeza lengo lao kubwa ni kuwawezesha kuwapatia mikopo pamoja na kuwajengea viwanda vidogo vidogo.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wajasiriamali wote walioshiriki katika maonyesho hayo Issa Njoka amesema kwamba serikali inapaswa kuhakikisha inawasaidia katika kuwaongezea mitaji sambamba na kuwasaidia kufanya maonyesho ya bidhaa wanazozitengeneza kuanzia ngazi za wilaya hadi Taifa ili waweze kutambulika zaidi.

Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na shirika la viwanda vidodovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani yamewashirikisha wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, morogoro, Lindi, Mtwara , pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani .
 Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage akiwahutubia wajasiriamali walioshiriki katika  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa  yaliyoendelea kufanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yameshirikishi jumla ya mikoa mitani ya kanda ya mashariki.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wa pili kulia akikata utepe na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakaati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya wajasiriamali kanda ya mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.
 Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage akiangalia moja na biadhaa ambazo zimetengenezwa na wajasiriamali hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...