THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea uwezo wasanii wetu na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wataalamu kutoka pande hizi mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

 “Kwa miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye

Mhe. Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua, kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya kufanya maonyesho kama haya nchini China.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.

 Kikundi cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.