Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 

Baraza jipya la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni (BLRC) limeagizwa kusimamia mfumo huo kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2013 ili kuondosha kasoro zilizojitokeza katika mfumo wa zamani na kurahisisha ufannyaji wa biashara Zanzibar.

Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali ametoa maagizo hayo Ofisini kwake Migombani alipokuwa akizindua Baraza hilo lenye wajumbe 13 kutoka Taasisi za Serikali na watu binafsi likiongozwa na Mwenyekiti wake Vuai Mussa Vuai.

Amesema mfumo uliokuwa ukitumika wa utoaji leseni za biashara ulikuwa sio rafiki kwa wadau, ni wenye unaurasimu na unachukua muda na pia unagharama kubwa katika upatikanaji wa baadhi ya leseni.

Ametaja kasoro nyengine za mfumo wa zamani wa utoaji leseni kuwa ni kuwepo kwa sheria na vyombo vingi vya utaji leseni, kutokuwepo msimamizi wa vyombo hivyo na kuwepo kwa aina tofauti za leseni, vibali au ruhusa ya kuendesha biashara ambazo zote zina lengo moja.

Balozi Amina amelitaka Baraza hilo katika kutekeleza majukumu yake kuondosha urasimu na kupunguza muda katika utaratibu wa kuomba na utoaji leseni, kusimamia utaratibu rahisi na wa kupunguza gharama katika upatikanaji wa leseni na kuwepo masharti ya kusimamia biashara.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akizindua Baraza jipya la Kusimamia Mfumo wa utoaji leseni Ofisini kwake Migombani, Mjini Zanzibar.
 Katibu Mtendaji wa BLRC Rashid Ali akitoa maelezo mafupi ya shughuli za Baraza hilo wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Waziri Amina Salum Ali Ofisini kwake Migombani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...