Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe kutoka Jeshi la Polisi,Kamishna Albert Nyamhanga akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...