.Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na viongozi mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu  wa kuendesha Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya NHIF leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu).
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) akitoa maelezo mafupi kuhusu shughuli za Mfuko leo makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

 MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar katika ziara ya mafunzo iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit Kombo ambaye ni Waziri wa Afya wa Zanzibar.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo, Waziri na timu yake walipata melezo na kujionea shughuli mbalimbali za Mfuko huo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema "tunahitaji kujifunza kutokana na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa kutosha".

Mh. Kombo alisema kuwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na  kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya kazi kwa karibu sana na hii inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya afya kwa pande zote.

Akiwakilisha mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya Tehama lakini pia mifumo  ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. "Pamoja na mambo mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja zao"alisema.

Akitoa shukrani zake kwa NHIF katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari, Waziri Kombo alishukuru Mfuko na kusema kwamba utabakia kwenye historia ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar lakini pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa kusema "Bima ya afya ni Mkombozi wa wanyonge"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...