Na Shamimu Nyaki-WHUSM. 

Ubalozi wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.

Hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.

“Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi. 

. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi.  





Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu (Katikati ) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw Gao Wei kutokana na msaada wa Vifaa walivyotoa kwa Wizara kwa ajili maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara Bibi Leah Kihimbi. 
Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (Kulia) akitoa neno la Shukrani kwa Ubalozi wa China hapa nchini baada ya kupokea Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Petro Lyatuu, na kulia ni Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw. Gao Wei. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...