Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na madini, Profesa James mdoe akizungumza na waandishi habari katika juu mkakati mpango wa gesi asilia leo jijini Dar es salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WIZARA ya Nishati na Madini iko katika hatua ya mwisho ya kutengeneza mpango mkakati wa matumizi ya gesi asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara na Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema mpango huo ni kuangalia matumizi ya gesi asilia kwa ndani ya nchi na kuweza kuchochea uchumi wa viwanda.
Profesa Mdoe amesema kuwa mpango mkakati utasaidia katika kutengeneza katika kuangalia soko la gesi asilia nje ya nchi.
Amesema kuwa matumizi ya gesi asilia kinatarajia kujengwa kiwanda kikubwa kinachotumia gesi hiyo.
Nae Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapuulya Naomba amesema kuwa wataanza na kusambaza mabomba katika jiji la Dar es salaam kutokana matumizi ya mkaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...