THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WLAC WAZINDUA AWAMU YA TATU YA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ JIJINI DAR

Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (katikati), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) wakiinua Vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni (kushoto) na Jackline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam, kwa pamoja wakiinua vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ iliyofanyika kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, leo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwacity Almas, akiimba na kucheza pamoja na baadhi ya kinamama waliohudhuria uzinduzi wa Awamu ya tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ ya Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), iliyozinduliwa leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Picha na Mafoto Blog