KAMPUNI ya Woolworths yenye maduka yakuuza nguo katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha, imemkabidhi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 20 ikiwa ni mchango wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.
 
Akizungumza wakati akipokea hundi hiyo, Waziri Mkuu aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada walioutoa kwa watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo lilisabisha vitu na uharibifu mkubwa wa mali mkoani Kagera.

Waziri mkuu alisema makampuni na biashara zinao mchango mkubwa katika kusaidia jamii na kuisufu kampuni ya Woolworths ambayo alisema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari ikisaidia jamii zenye mahitaji.
 
“Napenda kuishukuru kampuni ya Woolworths kwa kuguswa na tatizo lililowapata ndugu zetu wa Kagera na kuona umuhimu wa kutoa mchango huu.  Kampuni hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa pamoja na kusaidia jamii pia imekuwa ikiuza nguo zenye ubora,” alisema.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa wa kampuni hiyo Joehans Bushiri alimwambia Waziri Mkuu kuwa, ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kutenga sehemu ya faida yake kwa ajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji.

“Woolorths imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii zenye mahitaji kama yatima na makundi mengine. Msaada huu wa leo ni sehemu ya utaratibu tuliojiwekea kwa ajili ya kurudisha sehemu ya faida tunayopata kwa jamii zenye mahitaji maalum,” alifafanua.
 
Kampuni ya Woolworths ni moja ya makampuni makubwa Africa na duniani yanayojihusisha na uuzaji wa nguo na vitu vya aina mbali mbali vyenye ubora wa hali ya juu ikiwa na matawi mawili jijini Dar es Salaam na matawi mawili jijini Arusha.
 Waziri Mkuu Kasim Majaliwa (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Woolworths Tanzania Joehans Bushiri allipokuwa akitoa mchango wa hundi ya shilingi 20m/- ikiwa ni mchango wa kuchangia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera. Walio kaa kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara Charles Mwijage, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mwinyi Mvua na wa mwisho kulia ni Mkuu wa kitengo cha fedha wa kampuni hiyo Samson Katemi.
   Waziri Mkuu Kasim Majaliwa (wa kwanza kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi 20m/- kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Woolworths Tanzania Joehans Bushiri ikiwa ni mchango wa kuchangia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera. Wengine ni Mkuu wa kitengo cha fedha wa kampuni hiyo Samson Katemi na Waziri wa viwanda Biashara Charles Mwijage.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...