THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

YANGA YAENDELEA KUTOA DOZI LIGI KUU, YAICHAPA JKT RUVU 4-0 UWANJA WA UHURU LEO.

TIMU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya alama 24 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga walioanza kuona goli la JKT Ruvu dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Obrey Chirwa lakini umakini mbovu wa safu ya washambualiaji ulifanya wakose magoli mengi na mpaka kumalizika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga walitoka mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulisakama lango la JKT Ruvu na katika dakika ya 63 Amisi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliiandikia Yanga goli la pili na dakika ya 83 Simon Msuva kwa kutumia udhaifu wa golikipa Said Kipao aliyekuwa mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa Yanga akaweka kimiani goli la tatu.

Safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu wanashindwa kuwa makini ambapo wanashindwa kufanya mashambulizi ya uhakika na mabeki wa Yanga kuweza kusahihisha makosa yao.

Dakika ya 90, Amisi Tambwe anaiandikia Yanga goli la nne na kupeleka kilio zaidi kwa JKT Ruvu na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga wanatoka mbele kwa goli 4-0.

Yanga imecheza leo chini ya Kocha Juma Mwambusi baada ya Aliyekuwa kocha mkuu Hans Van De Pluijm kujiuzulu jana jioni.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia mara baada ya kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe akiachia mkwaju mkali uliotinga moja kwa moja wavuni na kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.
Mchezaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwania Mpira na Beki wa Timu ya JKT Ruvu, Nurdin Mohamed katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 4-0.


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    KUTAFUTA FURAHA MAISHANI NI KAMA KUMTAFUTA PAKA MWEUSI KATIKA CHUMBA CHENYE GIZA, YANGA MNATAKA FURAHA GANI ZAIDI YA HII, MNAMFUKUZA KOCHA WENU NA MKIJUWA KUWA WACHEZAJI WENU WAMEKAA PAMOJA MUDA MREFU NA MWALIMU WAO HUYO, LEO MNAFANYA KITU KIBAYA SANA, USHAURI WANGU MPENI HIYO KAZI YAKE, MTAANZA KUFUGWA HAPA BURE.

    DR, JAMESSY

  2. Anonymous Anasema:

    naona Yanga wamebadilisha njano yao kimyakimya