UONGOZI wa klabu ya Yanga umetuma barua ya maomb kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Visiwani Zanzibar kuomba kutumia  Uwanja wa Amani kwa ajili ya michuano yao mbalimbali na kuutumia kama uwanja wao wao wa Nyumbani.
Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii.

HATUA hiyo imekuja baada ya Serikali kuzifunia timu za Yanga na Simba kutumia Uwanja wa Taifa kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 01 kwenye mechi ya Ligi kuu ya Vodacom timu hizo zilipokutana na kusababisha kungolewa kwa viti na kuvunjwa kwa geti la kuingilia na mashabiki wa pande zote mbili.

Klabu ya Yanga imeandika barua hiyo na tayari imeshapokelewa na uongozi wa  Wizara husika visiwani Zanzibar, umeomba kutumia Uwanja huo kwa ajili ya mechi za ligi kuu na hata michuano ya Kimataifa itakapoanza.

Katibu mkuu wa ZFA Khasim Haji Salum amesema kwamba kwa upande wao kama uongozi  umekubaliana na jambo hilo lakini maamuzi kamili ya kuruhusiwa uwanja huo ni jukumu la Serikali ambao wao ndio wenye mamlaka kamili.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema wametuma barua tayari na wana imani kuwa majibu watayapata kwa kuda muafaka kabisa kwani kuanzia wiki ijayo ligi  taendelea tena na wanataka kutumia Uwanja huo na benchi la ufundi limeridhia kutokana na hali halisi ya Uwanja ulivyo.

Kutokana na maombi hayo, katika Kanuni za ligi kuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeweka wazi kanuni za ligi , “endapo timu yoyote haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mchezo wa ligi kuu inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa  jirani mkoa  wa timu husika ndani tya Tanzania bara ilimradi uwanja uwe na sifa zinazokubalika na uthibitishwe au kuidinishwa na TFF, baada ya uteuzi wa uwanja timu haitaruhusiwa kubadilisha uwanja  huo kinyume na sababu za kikanuni”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...