THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ZAIDI YA WAKAZI 5,000/-WANUFAIKA NA MRADI WA ELIMU YA UZAZI

Zaidi ya wakazi 5,000/=wa vijiji sita vya vya kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani wamenufaika na mradi wa elimu kuhusu  afya ya uzazi na mtoto iliyotolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana naTaasisi ya  uzazi na malezi bora (UMATI).

Takwimu hizo zilitolewa jana na  Razia Mamboleo Ofisa wa Programu wa mradi huo Wilayani hapa ambao umehusisha  vijiji vya Shela,Mohoro Mashariki,Mohoro Magharibi,Ndundutawa,King'ong'o  pamoja na Kwaijia.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za mradi huo Radhia alisema mradi huo umeleta mafanikio makubwa  ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto,akina mama kupata mwamko wa kuhudhuria Kliniki kwa wakati mwafaka kipindi cha ujauzito sambamba na kuboreshwa kwa huduma za uzazi  katika vijiji hivyo.
Mmoja wa Watoa elimu jumuishi(WAJA) Jumanne Mbondele,akielezea jambo kuhusiana na mwitikio na kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo,wakati Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo pamoja na Taasisi ya Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya kata ya Mohoro ,Wilayani Rufiji mkoani Pwani.


Aidha Radhia alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia mradi huo umefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi  sambamba na kuwapatia wanawake chanjo kwa wakati tofauti na awali .

Alijinasibu kuwa mradi huo umefanikiwa kutoa elimu kwa watoa huduma jumuishi (WAJA) ambao walipatiwa mafunzo kwaajili ya kuelimisha jamii jambo ambalo limeongeza uelewa wa masuala ya afya ya mama na mtoto katika jamii ya watu wa Rufiji.

Akizungumzia kuhusu changamoto za mradi huo ambao unafikia tamati Oktoba mwaka huu, Razia  alieleza kuwa  kikwazo kukibwa ni  ya kieneo na kijiografia ambayo ufikaji wake ni wa kusua sua. 
Baadhi ya watoa elimu jumuishi ya afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo, (WAJA) wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo pamoja na Taasisi ya Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya kata ya Mohoro ,Wilayani Rufiji mkoani Pwani.

"Changamoto kubwa ni ya kieneo, maeneo mengine hayafikiki kutokana na miundo mbinu mibovu ambayo imesababisha magari kutofika"alisisitiza Razia.

Kwa upande wake mmoja wa Watoa elimu jumuishi (WAJA) Jumanne Mbondele alisema mradi huo umepata mwitikio chanya  kwa wakazi wa Kata hiyo lakini changamoto kubwa ni ya kijiografia.

"Mwitikio ni mzuri sana na imesaidia sana Kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo lakini mradi ni wa muda mfupi na ndiyo kama hivyo uanelekea ukingoni,tuanaomba mradi uongezewe muda angalau uwe wa miaka mitatau ili uweze kufikia maeneo mengine"alihitimisha Mbondele.
Baadhi ya wakina mama wakisuburi huduma za afya katika kituo cha Afya Mohoro,Wilayani Rufiji mkoani Pwani kituo hicho kinafadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi wa Afya ya baba mama na mtoto na kuendeshwa na Taasisi ya Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya kata ya Mohoro ,Wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Naye Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kuwa  mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa  hasa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, afya ya mama na mtoto sambamba na matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanaume na wanawake.

"Vodacom Tanzania Foundation itaendelea kusaidia jamii hasa katika masuala mazima ya afya  ili kutimiza malengo ya milenia kuhakikisha sera ya afya ya kupunguza vifo vya mama na mtoto sambamba na uboreshwaji wa afya ya uzazi "alihitimisha Rwehikiza.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mohoro,Tegemei Mtambo(kushoto)akielezea jinsi watoa elimu jumuishi(WAJA) pichani walivyochangia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa elimu ya afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo,wakati Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo na kuendeshwa na Taasisi ya Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya kata ya Mohoro ,Wilayani Rufiji mkoani Pwani.