THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ZIMEBAKI SIKU 15 MSHINDI WA MILIONI 100/-KUPATIKANA KUPITIA KAMATA MPUNGA.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akimuonesha namba ya simu Afisa mwandamizi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Humudi Abdulhussein(kulia)ili aihakiki kabla ya kumpigia mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/- Bw. Joseph Machima, Mkazi wa Sengerema Mkoa wa Mwanza aliyeibuka mshindi wakati wa kuchezesha droo ya  wiki ya promosheni ya ”kamata mpunga” inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544.Aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
Kushoto ni Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa kampuni hiyo, Neema Mgombelo.
Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa Vodacom Tanzania, Neema Mgombelo(kushoto)na Afisa mwandamizi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Humudi Abdulhussein(kulia) wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(katikati)akiongea kwa simu na mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/- Bw. Joseph Machima, Mkazi wa Sengerema Mkoa wa Mwanza aliyeibuka mshindi wakati wa kuchezesha droo ya  wiki ya promosheni ya ”kamata mpunga” inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544.Aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

Zikiwa zimebakia siku 15 kwa promosheni ya”Kamata Mpunga”kuisha na mshindi mmoja wa droo ya mwisho atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 100. Leo hii  mkazi wa Moshi mjini Hassan Ochieng amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 20/= na Mkazi wa singida mjini ambaye ni muuza mitumba Bw. Aman Manyenye amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5/= pamoja na Joseph Machima,Mkazi wa Sengerema Mkoa wa Mwanza.

“Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ametoa wito kwa wateja wa kampuni hiyo na watanzania wote kwa ujumla ambao hawajajiunga na mtandao huo waweze kujiunga na kuchangamkia frusa hii yakipekee kabisa kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/- na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na mwisho wa mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/=

Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi  300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”.

maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi.

Kuna wateja wengine hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni hii wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa kiasi cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila watakuwa wameingizwa kwa droo moja kwa moja.

v  Mpaka sasa jumla ya washindi 327 wamejinyakulia fedha mbalimbali tangu kuanza kwa promosheni hii.

v  Washindi 297 wamejishindia Milioni mojamoja kila mmoja

v  Washindi 18 wa wiki wamejishindia shilingi Milion 5/5 kila mmoja

v   Pia washindi 4 wameondoka na  kitita cha shilingi Milioni 20/-