Na Daudi Manongi,MAELEZO. 

Wizara ya Fedha na Mipango imeanza zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo katika mkoa wa Pwani, Kibaha. Uhakiki huu hautausisha wastaafu wanaolipwa kupitia mifuko ya hifadhi za jamii kama vile PSPF, NSSF, PPF na GEPF.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango huo wa uhakiki ulioanza leo mkoani Pwani.

“Uhakiki huu unatokana na utaratibu uliojiwekea Wizara ya Fedha na Mipango wa kufanya uhakiki wastaafu ili kuhuisha orodha ya malipo ya wastaafu na inasaidia kubaini mabadiliko ya taarifa za wastaafu kama vile kufariki na hivyo kuepuka kulipa wasiostahili”Alisema Bw.Mtonga.

Aidha akizungumzia kuhusu utaratibu wa uhakiki huu amesema kuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima na limeanzia katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha na litafanyika kuanzia leo tarehe 10 mpaka tarehe 14 mwezi huu na kuendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa pwani mpaka tarehe 21 mwezi huu.

Baada ya uhakiki katika mkoa wa Pwani zoezi litaendeshwa kikanda nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Katavi kuanzia tarehe 31 Octoba mpaka tarehe 11 Novemba mwaka huu.

Pia zoezi litafanyika katika kanda ya kati likijumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida kuanzia tarehe 21 mpaka 25 Novemba.

Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa wazee wastaafu Bw.Benedict Kalaguza amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kufanya uhakiki huu wa wastaafu na kwamba zoezi limekuwa ni zuri lisilokuwa usumbufu wowote na limeboreshwa zaidi kwa kutumia teknolojia nzuri zaidi.

Aidha Wastaafu wanaohakikiwa wanatakiwa kufika kwenye vituo hivyo wakiwa na nyaraka kama Kadi ya Benki, Picha za passport mbili, Barua ya Ajira ya Kwanza, Barua ya Kustaafu au kupunguzwa kazi kazini, barua ya Tuzo la Kustaafu, Nakala ya Hati ya Malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, kitambulisho cha pensheni na barua ya Kudhibitishwa kazini.
Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Bi Joan John akimwelekeza Bw.Benedict kalaguza jinsi ya kujaza fomu za uhakiki wa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.Zoezi hilo limeanzia mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha leo na litafanyika nchi nzima. 
Baadhi ya wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki mkoani Pwani.Uhakiki huu unahusisha wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Je wastaafu waliohushi vyeti vya elimu watafanywaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...