THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Airtel yazindua huduma za mawasiliano Lindi Vijijini


Huduma hizi mpya za mawasiliano zitawafikia wakazia wa vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo kwa kuwahakikishia wakazi wote wa Lindi vijijini huduma za mawasiliano za uhakika, huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na hatimae kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema “ tunayofuraha kupata huduma za mawasilino hapa cheleweni na vijiji vya jirani. Airtel kwa kuzindua mnara huu, serikali tunaungano jitiada hizi za kuboresha mawasiliano huku vijiji kwa sasa wakazi wa vijiji hivi mtaweza kutumia huduma ya mawasiliano kwa kufany a biashara zenu za nazi kwa kujitafutia masoko sehemu nyingine lakini pia itasaidia kuondoa tatizo lakutembe na fedha nyingi pale mnapofanya biashara kwa kuwa mtatumia huduma za kifedha za Airtel Money kujichukulia fedha zenu wakati wowote

Mkuu wa wilaya aliongeza kwa kusema “Mawasiliano haya yatasaidia sana wilaya yangu katika kukuza elimu kwa kuwa nitaweza kuwawasiliana na watendaji wangu wote wakati wowote. Sasa nitoe tamko kwamba nimeongea na Airtel ili kutuma ujumbe wa meseji kwa wazazi wote kwa kuwa ndio mtandao unaotumika na wengi hapa katika vijiji vyetu vya ng’apa ng’apa kuhusu kuandikisha watoto wote waliomaliza shule za msingi waende sekondari, Airtel wamenikubalia sasa ikiwa mzazi atakaidi kuitikia wito nitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfunga”.

Nataka kuona huduma hii ya Mtandao wa Airtel tunayoizindua leo inaleta tija katika shughuli za uchumi kama vile uzalishaji wa korosho, kusaidia biashara ndogo za kati na kubadilisha maisha ya jamii kwa ujumla. Napenda kuchukua fursa hii kuwahasa wakazi pia kuilinda miundombinu ya mawasiliano haya ili yaduma. Alimalizia kusema Mh, Ndemanga

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel, Saleh Saphy “Tunayofuraha kutoa huduma za uhakika na gharama nafuu nchi nzima, kwa wakazi wa Lindi , tunawahakikishia ofa kabambe za msimu huu wa sikukuu kupitia ofa yetu maalumu ya “Wadatishe” ambayo mnaweza kupata simu orijino kwa gharama nafuu hadi ya shilingi 79,000 tu.-. vilevile wateja wanaweza kupata vifurushi vya intaneti vya 1G kwa shilingi 1000 wakati huu wa msimu wa sikukuu .

Kupitia huduma ya mawasiliano wateja wataunganishwa na huduma za intaneti, huduma za kifedha za Airtel Money kutuma na kupokea pesa, kupiga simu wakati wowote, kusajili simu zao na pia kupata nafasi ya kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao. Hizi ni baadhi tu za huduma zetu hivyo natoa wito kwa wakazi wa cheleweni, Ng’apa na Michee kujiunga na timu ya Airtel SIBANDUKI na kufurahis huduma zetu.” Alisisitiza Saphy
Kulia ni mkuu wa wilaya Lindi bw, Shaibu Ndemanga akikata utepe na akishangiliwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui, Afisa tawala wilaya Lindi Mh, Thomasi Safari na Meneja Mauzo wa Airtel Bw, Saleh Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
Mkuu wa Wilaya Lindi bw, Shaibu Ndemanga akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui na Meneja Mauzo wa Airtek Bw, saleh Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
Kushoto Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akielezea huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa kijiji cha Cheleweni kwa Mkuu wa wilaya Lindi bw, Shaibu Ndemanga (wapili kulia) mara baada ya kuzindua mnara huo huku wananchi wakisikiliza. katikati ni Meneja wa Airtel Lindi by Saleh safy. Airtel imejenga mnara huo kutoa mawasiliano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii.

Katika juhudu za kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia maeneo ya pembezoni mwa nchi, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wake wa mawalisiliano na kuanzisha hduma za simu kwa mara ya kwanza katika kijiji cha cheleweni mkoa wa Lindi.