Zaidi ya wanawake 500 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi hayo (ZCA), Ilala Afya Centre ya Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar.

Kampeni hiyo ya siku moja iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja iliwashirikisha akinamama wenye umri kuanzia miaka 25 ilikuwa na lengo la kuweza kuwagundua mapema akinamama wenye tatizo la maradhi hayo ambayo dalili zake zinachelewa kujitokeza.

Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa ZCA Dkt. Msafiri Marijani amesema kampeni hiyo ilihusisha uchunguzi wa Utrasound na uchunguzi wa sindano na waliopatikana na dalili watafanyiwa vipimo ili kujua kama ni saratani ama matatizo mengine.

Dkt. Marijani amekumbusha kuwa saratani hadi hivi sasa haina tiba na kitu muhimu ni kuigundua mapema ili kuidhibiti kabla haijaleta athari kubwa hivyo amewashauri wananchi kupima afya zao mara kwa mara.

“Saratani ni maradhi yanayouwa watu wengi duniani kutokana na kuchelewa kugundulika mapema, kitu muhimu ni wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao,” alisisiti Dkt. Marijani.Amesema Hosipitali zote za Wiala na vituo vingi vya Afya vya vijijini vinatoa huduma ya uchunguzi wa saratani hivyo amewashauri wananchi kuvitumia.

Kiongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya saratani Zanzibar Bi. Zakia Mohd amesema kufuatia uchunguzi huo ambapo zaidi ya wanawake 100 wamebainika kuwa na dalili za saratani, wamegundua kuwa tatizo ni kubwa kinyume na walivyo fikiria awali.Amesema kutokana na hali hiyo ZCA itafikiria kununua chombo maalumu cha uchunguzi ‘mamography’ ambacho kinauwezo wa kugundua dalili za awali kabisa za maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Jumuiya imeazimia kufanya uchunguzi mwengine wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tenzi dume katika siku zijazo kwa vile ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbuwa wananchi wengi wa Zanzibar. Mwisho

Baadhi ya akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa hospitali hiyo.

Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee (kulia) akibadilishana mawazo na viongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na saratani Zanzibar (ZCA) ambapo taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeandaa kampeni hiyo.

Dak. Nalvis Dominguez Torres akimfanyia uchunguzi wa maradhi ya saratani ya matiti mmoja wa akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi hayo.

Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar Msafiri Marijani akichukua sampuli kutoka kwa mmoja wa akinamama waliofika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa saratani.

Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee akitoa maelekezo kwa akinamama waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti katika kampeni iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa kituo hicho, Wizara ya Afya na ZCA. icha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ndio ni katika uchunguzi na tiba kwa jumla hakuna jinsi, lakini nadhani kama walivyoweza kujistiri nyuso zao ili wasitizamane au kuonana uso kwa macho na hao matabibu au kwa sababu nyinginezo kama zipo. Basi hata kwa sisi wapitiaji wa ukurasa huu, mngezingatia stara picha ya tatu na ya nne kama hakukuwa na ulazima wa kuziweka hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...