Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda amezishauri hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali kuboresha huduma za afya ili wananchi waliojiunga katika mifuko ya afya ya jamii (CHF) na mfuko wa bima ya afya washawishike kutumia huduma katika hospitali zao.

Makinda ametoa rai hiyo alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa na changamoto zilizopo ili kwa ushirikiano wa mfuko wa bima ya afya na wadau wake waweze kuzitatua.

Amesema hospitali na vituo binafsi au vya mashirika mbalimbali wamekuwa wanufaikaji wakubwa wa kupata wateja wengi wa bima ya afya na mifuko ya afya ya jamii kutokana na kusifiwa kuwa wanatoa huduma bora tofauti na hospitali za serikali ambazo hupata wateja wachache na hivyo kupata faida kidogo.

Makinda amesema hamasa anayoitoa ya kuboresha huduma kwa vituo vya serikali haimaanishi mfuko wa taifa wa bima ya afya hauthamini vituo na hospitali binafsi bali inataka hospitali za serikali kuboresha huduma na kuingia katika ushindani.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda katikati kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mtahew John Mtigumwe na kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo, wa kwanza kulia ni meneja Mfuko wa Bima ya Tifa Mkoa wa Singida Bwana Adamu Salumu.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akikagua hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida, mwenye tai nyekundu ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akikagua hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida,kulia kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta Ramadhani Kabala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...