Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Baada ya kuanza safari zake Octoba 14 2016,Shirika la Ndege la ATCL limekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa ndege na kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

Akitoa changamoto hizo,Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,Mhandisi Emmanuel Korosso amekili kuwepo kwa changamoto ya Marubani katika Shirika hilo ikizingatiwa mpaka sasa Shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya Marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

Amesema kuhusu Wafanyakazi Bodi yake imeagiza Menejimenti ya Shirika kusimamisha kwa muda mkataba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

"Katokana na haja ya kuboresha Utendaji, ATCL iliamuliwa Wakurugenzi wote katika Menejimenti ya ATCL isipokuwa Mkurugenzi Mtendaji,na baadhi ya Menejimenti waondolewe katika nafasi zao Mara moja kutokana na Utendaji dhaifu na viwango vya Elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao",amesema Mhandisi Korosso

"Tumeamua wakurugenzi wanaokaimu nafasi zao warudishwe katika nafasi zao za chini ambazo siyo za Menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani",ameeleza Mhandisi Korosso.Aidha,Wakurugenzi na Menejimenti waliokuwa wamethibitishwa tumeagiza waondolewe ATCL ili wapangiwe majukumu mengine kulingana na sifa zao.

Aidha Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi zote za Wakurugenzi na pia nafasi za Mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na Bodi (Interim Organization Structure).Pia Mtendaji Mkuu ameagizwa kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuna umuhimu wa kuajiri watu wengine kutokana na utendaji usioridhisha wa wafanyakazi wanaoshikiria nafasi hizo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL,Mhandisi Emmanuel Korosso(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ofisi za Shirika hilo,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika,Ladislaus Matindi,kulia ni Mjumbe wa Bodi,Dkt. Mussa Mgwata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...