Wananchi wa Shehia ya Mtofaani Masingini ndani ya Jimbo la Welezo wameiomba Serikali Kuu kufikiria maombi yao ya kutaka kupewa eneo lililokuwa likimilikiwa na Kikosi cha Kuzuia Magendo { KMKM } kwa ajili ya kulitumia kwa shughuli zao za Kijamii.

Wamesema eneo hilo ni sehemu pekee iliyowazi kwa shughuli za Kijamii katika shehia ya Mtofaani ambalo linaweza kuwasaidia kwa ujenzi wa Soko,huduma za Afya, Skuli na Michezo ili kuwaondoshea usumbufu Watoto na Wananchi kufuata huduma hizo katika Masafa marefu. 

Wananchi hao walipaza sauti zao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua eneo hilo baada ya kupokea kilio chao wanacholalamikia eneo hilo kumilikiwa na Mtu aliyetambulika kwa jina Moja tu la Zahor ambae kwa sasa ameshaamua kulizunguushia Ukuta eneo lote.

Walieleza kwamba muda mrefu uliopita  Kamati ya Maendeleo ya Eneo hilo kupitia Sheha wa Shehia hiyo iliwahi kupeleka maombi yao ili kupatia eneo hilo lakini jitihada hizo hazikufanikiwa na badala yake kushuhudia ugawaji wa Viwanja uliopelekea kuwavunja moyo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akilikagua eneo liliopo Mtofaani kwenye Makutano ya Bara bara za Hawaii na Masingi ambalo liliombwa na Wananchi kwa shughuli za Kijamii lakini kwa sasa kuna tetezi ya kumilikiwa na Mtu mwengine.
 Balozi Seif akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tawi la Mofaani Bwana Iddi Sultan kuhusiana na utata wa eneo hilo linalomilikiwa na mtu binafsi hivi sasa.
  Balozi Seif  kushoto akiwa nyuma ya Ukuta wa Matofali uliojengwa kati kati ya eneo hilo akijaribu kuangalia upande wa Pili wa eneo hilo lenye utata wa umiliki. Aliyepo upande wa Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Mheshimiwa Hassan Khamis Hafid.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...