WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Dola za Marekani 33,000 (sawa na sh. milioni 71) kutoka kwa makampuni ya Kuwait ili ziwasaidie wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo (Jumatano, Novemba 9, 2016), Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Bw. Jasem Al-Najem amesema msaada huo ni mchango kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim, Bw. Fouad Alghanim aishiye Kuwait.Amesema watu kadhaa wameguswa na maafa yalitokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu na wameamua kuchangia ili kuisaidia juhudi za Serikali kukabiliana na hali hiyo ambayo haikutarajiwa.

“Tunatambua kuwa kazi ya kurejesha huduma kwa wananchi ni kubwa, na Serikali peke yake haiwezi kubeba mzigo wa kukarabati miundombinu na majengo ya ofisi na makazi ili kuurejesha mkoa huo katika hali yale ya kawaida,” amesema.

Akizungumza na Balozi Al-Najem ofisini kwake Bungeni, mjini Dodoma, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Tanzania imeguswa na moyo wa upendo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim na wenzake.Akitoa shukrani kwa msaada huo, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha mchango huo unafikishwa Kagera kwa walengwa.

Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Septemba 10, mwaka huu lilisababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa. Pia lilisababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya dola za Marekani 33,000 kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyka ofisini kwa Waziri Mkuum bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...