THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL NAJEM ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE


Na Anna Nkinda - JKCI

Serikali ya Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine  na vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika katika chumba cha upasuaji.

Ahadi hiyo imetolewa leo na  Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem Al Najem alipotembelea  Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia ni  jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa  tiba.

Mhe. Balozi Al Najem alisema vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu vitapatikana kabla ya kumalizika  kwa mwaka huu ambapo vifaa  pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017.

“Serikali ya nchi yangu inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii pamoja na Taasisi zingine zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini ili watanzania waweze kupata huduma bora”, alisema Mhe. Balozi Al Najem.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi  alishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na mashine  zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa moyo.

“Tuna vyumba vitatu vya upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina vifaa, kupatikana kwa vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait kutatufanya tuwe na vyumba vya upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia  kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .

Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kutoa  zawadi kwa watoto waliolazwa.
Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.