Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alipotembelea katika ofisi za Wizara hiyo.

Balozi Sarah alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi kwa kipindi kifupi. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na Mpango wa Serikali kupanga, Kupima na Kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini pamoja na Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) ambao unalinga kutoa huduma za ardhi kwa wananchi kielektroniki pamoja na utoaji hati za kielektroniki.

Aidha, Balozi huyo amepongeza mchakato wa kuandaa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 2016 na jinsi ulivyo shirikisha wananchi na wadau wote wa sekta ya ardhi nchini.

Mhe. William Lukuvi alimueleza Balozi huyo ambaye alifurahishwa zaidi na juhudi za Serikali za kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi katika kujiletea maendeleo yao, pamoja na juhudi za kuwawezesha wananchi wanaoishi katika makazi holela kupimiwa na kumilikishwa makazi yao pamoja na kupatiwa hati miliki za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akielezea kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Afisa Maendeleo kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania wakati akimuaga Balozi wa Uingereza nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...