THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BANK YA NMB YAKABIDHI VITANDA ,MAGODORO NA MADAWATI TUNDURU

 Meneja wa Bank ya NMB kanda ya kusini Bi Lilian Mwinula akikabidhi vitanda tisa ,magodoro tisa kwa mkuu wa wilaya ya tunduru Juma Homera kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa hospital ya Wilaya ya Tunduru.
--------------------------------
Bank ya NMB tawi la TUNDURU mkoani RUVUMA imekabidhi msaada wa vitanda 9 na magodoro 9 katika hospital ya wilaya ya tunduru pamoja na madawati 50 katika shule ya msingi majengo iliyopo mjini tunduru vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi, ikiwa ni shemu ya bank hiyo kurejesha kiasi cha faida inayopata kwa jamii kusaidia huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma homera  aliyeshika mikono kwa mbele akiongea na mmoja kati ya wagonjwa waliolazwa katika hospital ya wilaya ya tunduru.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Majengo wakiwa wamekaa katika madawati ambayo yametolewa na bank ya NMB tawi la TUNDURU lilipo wilayani humo.
KWA HABARIZAIDI HII HAPA ANGALIA RUVUMA TV on line.