THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Barclays na PEN Tanzania wazindua maabara ya Kompyuta inayotembea kusaidia shule za sekondari za serikaliMeneja Mawasiliano wa Barclays Tanzania, Hellen Siria, akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa tatu kulia), Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya (katikati mwenye miwani), na Mkurugenzi wa asasi ya PEN Tanzania, Sharnel Deo (wa nne kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kulia) akikabidhi pedi za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Wilaya ya Kinondoni mara baada ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya.
Ofisa Masoko wa Benki ya Barclays, Nasikiwa Berya (wa tano kushoto), akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya ya Kinondoni. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa PEN Tanzania, Nancy Kataraihya, Meneja Mawasliano wa Barclays, Hellen Siria na Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya.