THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Benki ya CRDB kufungua matawi mapya 11 kabla ya mwisho wa mwaka huu

Benki ya CRDB imesema imeshangazwa na habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa iko mbioni kufunga baadhi ya matawi yake kutokana na ukata. 
Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt.  Charles Kimei alisema kuwa hakuna ukweli wowote kwenye taarifa hizo, kwani hivi sasa Benki ya CRDB ipo kwenye hatua za mwisho za  kufungua matawi mapya 11. Hii ikiwa ni muendelezo wa sera yake ya kuhakikisha kuwa inafikisha huduma karibu zaidi na wateja.
“Nimeshangazwa  sana habari hizi za upotoshaji, ukweli ni kuwa mwaka jana (2015) tulifungua matawi 76 na kuajiri wafanyakazi 450. Mwaka huu (2016) tumeshafungua matawi 51 na tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha matawi mengine 11.  Hii itafikisha jumla ya matawi mapya 62 na jumla ya  ajira mpya 600 kwa mwaka huu tu. Takwimu hizi zinaonyosha kuwa Benki ya CRDB inaendelea kuimarika na kuwa Benki kubwa zaidi nchini na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.
Dkt. Kimei aliyataja matawi hayo mapya kuwa ni Muheza na Handeni (Tanga), LAPF (Dodoma), Ruangwa (Lindi), Soko la Mwanjelwa (Mbeya), Chato (Geita), Tarakea (Kilimanjaro), Mkwawa (Iringa), Mikumi (Morogoro), Wete (Pemba) na Kigamboni-Dar es Salaam.

“Naomba kuwatoa hofu wateja wetu juu ya taarifa zozote zenye lengo la kutuchafua kwani Benki  ya CRDB iko vizuri na inategemea matokeo makubwa ya kifedha ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016” alisema Dokta Kimei.