Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar   .
                
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.

Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib  Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa  bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.

Amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.

Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.
  Wafanyakazi wa gari ya mizigo wakishusha bidhaa zilizoharibika katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja tayari kwa kuangamizwa katika zoezi ililosimamiwa na Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika maandalizi ya kuharibu chakula na dawa zilizoharibika na kupitwa na wakati katika dampo la Kibele.
 Magari ya mizigo yakishusha shehena za bidhaa mbovu zilizokamatwa na maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi katika maghala na maduka Zanzibar.
 Mkuu wa operesheni wa uangamizaji wa bidhaa mbovu wa ZFDB ndugu Abdulaziz Shaib Mohd akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuangamiza bidhaa hizo katika dampo la Kibele
Kijiko cha Manisapaa ya Zanzibar kikiharibu bidhaa mbovu na zilizomaliza muda wake wa matumizi katika dampo la Kibele Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...