Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.

Na BMG

Maulid amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimili za wasanii wa filamu nchini.
Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa bodi hiyo pamoja na wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
Zaidi ya wasanii 300 wa Filamu mkoani Mwanza wakifuatilia warsha ya mafunzo ya filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...