THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BODI YA UTALII NA ATCL WAINGIA MKATABA WA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BODI ya Utalii nchini (TTB) na Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) limeingia mkataba wa pamoja leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni lengo la kukuza soko la Utalii wa ndani na kuongeza pato la taifa nchini.
Akizungumza baada ya makabidhiano ya mkataba huo baina ya mkurugenzi wa TTB DevotAha Mdachi  na Mkurugenzi wa TTB  Laislaus Matindi, Mwenyekiti wa TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa uwepo wa shirika la ndege la ATCL litasaidia katika ukuaji wa sekta ya utalii nchini kwani italeta chachu kwa watalii wa ndani na wa nje kuja kwenda kwa wingi.
Mihayo amesema kuwa TTB iliathirika kwa kiasi kikubwa sana hasa baada ya kutokuwepo kwa shirika la ndege na kutoa pongezi kwa juhudi zilizofanywa na Rais wa awamu ya Tano John Magufuli kwa kuirejesha upya na kuiwezesha kuwa na ndege zake zinazojiendesha zenyewe.
"Kwa juhudi zilizofanywa na Rais John Magufuli za kurejesha uhai kwa kampuni ya ATCL na kupata ndege zake ambazo zitasaidia kwenye kuutangaza utalii kwa watalii wa ndani na nje kwani itasaidia pia kuinua na kukuza pato ;la taifa kwa kuingiza fedha za kugeni,"amesema Mihayo.
Mkataba huo utakaowawezesha TTB kujitangaza Zaidi utawawezesha abiria watakaokuwa wanasafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini kupata vipeperushi vilivyozinduliwa leo vinavyoelezea baadhi ya vivutio vya utalii pamoja na kuoneshwa kwa vituo hivyo kupitia TV za kwen ye ndege kuvionyesha.
Mwenyekiti wa Shirika la ndege la ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso amesema kuwa kwa safari za ndani katika mikoa mbalimbali, pia kwa sasa ATCL inataka kuongeza safari za ndege kwenda katika mikoa mingine.
  
Kuongezeka kwa safari hizo, pia kutachangia kwa watalii kutumia ndege za serikali na kusaidia kuinua uchumi wa nchi na utakuwa ni endelevu ili kuimarisha ushirikiano hiuo.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akikabidhiana mkataba  na Mkurugenzi wa ATCL Laislaus Matindi wakishuhudiwa na  Mwenyekiti wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la ndege la ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso leo Jijini Dar es salaam. Chini wakiwa wanaweka saini ya makubaliano ya mkataba huo wakishuhidwa na mawakili wa pande zote mbili.


  Mwenyekiti wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Kulia)pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la ndege la ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso  wakionesha vijarada vya Utalii vilivyozinduliwa leo Jijini Dar es salaam vitakavyokuwa vinapatikana katika ndege za Shirika la ATCL.
 wakurugenzi kutoka shirika la ndege la ATCL na bodi ya Utalii TTB wakiwa wanafuatilia kwa makini mkutano huo.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Shirika la Ndege la ATCL na Bodi ya Utalii TTB baada ya kumalizika kwa utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.