CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka Viongozi na Watendaji wa
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Tanzania kuongeza juhudi katika
kuimarisha Chama ili kiweze kushinda na kuendelea kuongoza dola katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Rai
hiyo imetolewa na Katibu wa Idara ya Organazesheni Afisi Kuu Zanzibar,
Nd. Haji Mkema wakati akizungumza na Watendaji wa Jumuiya hiyo kwa ngazi
za Mikoa na Wilaya za Unguja Kichama katika ziara ya kuimarisha uhai wa
Chama katika jumuiya hiyo.
Alisema
jumuiya hiyo inatakiwa kuandaa mapema mipango endelevu ya kuimarisha
chama kwa kuongeza wanachama wapya ndani ya chama na Jumuiya kwa lengo
la kufanikisha ushindi wa CCM wa mwaka 2020.
Nd.
Mkema alieleza kwamba lengo la ziara hiyo ni kuwakumbusha viongozi na
watendaji wa UWT, majukumu ya msingi yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa
haraka ili kuhakikisha CCM inaendelea kubaki na hadhi yake ya
kusimamisha Dola inayojali misingi ya Demokrasia, Haki na utawala wa
kisheria.
“
Chama Chetu kinajivunia kuwa na jumuiya imara ya Akina Mama ambayo
imekuwa mstari wa mbele kutetea na kupigania maslahi ya CCM bila ya hofu
katika mapambano ya Kisiasa nchini, na kupata ushindi wa kishindo
unaotokana na ridhaa halali ya wananchi”., alisema Mkema na kusisitiza
kuwa Watendaji wa jumuiya hiyo wanatakiwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu
juu ya kasoro ndogo ndogo zilizomo katika jumuiya hiyo ili kuongeza
ustawi wa CCM kisiasa nchini.
Alisema
kwamba Akina Mama ndio nyenzo muhimu ya kisiasa kwa chama hicho hivyo
wanatakiwa kuendea na harakati za kujenga ushawishi kwa akina Mama
wenzao waliopo katika makundi na vyama mbali mbali kujiunga na Chama
hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...