THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DKT. KALEMANI AFANYA ZIARA KATIKA KITUO KIPYA CHA KUPOOZA UMEME CHA KURASINI NA MRADI WA KUSAMBAZA GESI MAJUMBANI

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji  wa kampuni ya Fichtner  ya Ujerumani na Shirika la  Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kufanya ziara katika  Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini kinachojengwa kupitia Mradi wa TEDAP ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake jijini  Dar es Salaam.
 Mtaalam kutoka Kampuni ya Fichtner ya   Ujerumani, Matthias Albers (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Katikati ni Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini, kinachojengwa chini ya Mradi wa TEDAP.
 Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (kulia) akitoa maelezo  kwenye kituo cha kuendesha mitambo (control  room) katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (katikati) akisisitiza jambo katika sehemu ya kupokelea laini za umeme.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ZAIDI