Na Theresia Mwami TEMESA Njombe.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu ameahidi kuwapatia makasha yenye vitendea kazi vya karakana pamoja na mashine ya kucharge betri za magari kwa wafanyakazi wa kituo cha TEMESA Mkoani Njombe.

Dk Mgwatu amesema kuwa ameamua kuleta mabadiliko katika ufanyaji kazi kwa kuhakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Nitaleta vifaa vinavyohitajika nataka kila mmoja atimize wajibu wake, tufanye kazi kwa kuzingatia uadilifu sababu tunabeba dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya viongozi mbali mbali wa serikali” alisema Dkt Mgwatu.

,Mtendani huyo ameongeza kuwa atokuwa na msamaha na mtumishi yeyote atakayeshindwa kuwa muadilifu na kutoimiza wajibu wake ipasavyo. Aidha Dkt Mgwatu aliwaagiza watumishi wa kituo hicho kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi zaidi na kuongeza pato la kituo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga alimueleza kuwa kituo kinakabiliwa na tatizo la madeni kinayodai wateja wake pamoja na madeni kinayodaiwa na wazabuni mbali mbali.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Musaa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo nyanda za juu Kusini ili kubaini changamoto mbali mbali zilizo kwenye vituo hivyo na kuzitafutia ufumbuzi.



Watumishi wa TEMESA Njombe wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa  Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (Mwenye shati la rangi ya bluu) alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Njombe.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto), akimsikiliza Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga (kulia) wakati alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...