THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DKT SHEIN AZINDUA HOSPITALI YA ABDALLA MZEE MKONI PEMBA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkurugenzi wa huduma za Hospitali Mohamed Dahoma na Viongozi wengine wakiwa katika chumba cha uchunguzi wa matatizo ya uti wa mgongo baada ya kuizindua rasmi Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo ,[Picha na Ikulu.] 26/11/2016.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Juma Malik Akil wakifuatana na Viongozi wengine wakati alipotembelea Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid hospitali hii imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid hospitali hii imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba na Viongozi mbali mbali baada ya kuizindua Hospitali ya Abdalla Mzee leo ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Dr.Shein, Mhe:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar. Npenda kukupongeza wewe binafsi na watendaji wako katika kuhakikisha huduma za afya kwa Wazanzibari na haswa kwa tukio hili wakazi wa Pemba. Naomba pia nimpongeze jembe mchapakazi Mhe;Mahmood Kombo Waziri wa Afya. Kwa heshima na taadhima naomba nikukumbushe Mheshimiwa muhakikishe upatikanaji wa huduma za PHYSIOTHERAPY katika Hospitali hiyo. Wakaazi wa Pemba tunasafiri mpaka Dar Es Salaam au hata mbele zaidi kufuatia huduma hizo. Kuna vijana tele wako wanaoweza kusomea huduma hizo kama ilivyokuwa zamani kusomeshwa hapahapa Tanzania kule KCMC. Tufanyieni kwa hili kwani tunateseka baba. Huduma za Physiotherapy tafadhali. Ahsante kwa heshima na taadhima kama nilivyoanza.