Na Mathias Canal
Ndugu zangu kama ambavyo tunakumbuka Tarehe 10/09/2016 majira ya saa 9 na dakika 27 Alasiri maeneo ya Kanda ya ziwa hususan  Mkoani Kagera kulitokea tetemeko la ardhi linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter ambapo Kitovu cha tetemeko hilo ni kwenye makutano ya latitudo 10 06’ na longitudo 31055’ eneo ambalo ni kilomita 20 kaskazini mashariki mwa kijiji cha Nsunga na kilomita 42 kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba na Kitovu hicho kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi kwenye eneo hilo.
Tetemeko hilo la ardhi liliacha familia kadhaa zikiwa na huzuni kubwa kwa kuwapoteza ndugu, jamaa na rafiki zao ambapo idadi ya watu waliofariki walikuwa ni 17 huku watu 560 wakipatiwa matibabu kutokana na majeraha waliyoyapata sambamba na kukutikana kwa uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi.
Kwa Mujibu wa Mtendaji Mkuu, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) alieleza sababu za kutokea kwa Tetemeko hilo la ardhi kuwa ilikuwa ni kutokana na kitovu cha tetemeko hilo kuwa kiko chini sana ya ardhi (Km 10) na kwa kutafasiri umbile la mawimbi ya tetemeko hilo yaliyonakiliwa na vituo vya kupimia matetemeko ya ardhi inaonekana kuwa tetemeko hilo limetokana na misuguano ya mapange makubwa ya ardhi iliyopasuliwa na mipasuko ya ardhi mithili ya mipasuko kwenye bonde la ufa. 
Kwa kuwa eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi liko karibu na mkondo wa magharibi wa bonde la ufa la Afrika Mashariki inakisiwa kuwa mtetemo huo ulisababishwa na kuteleza na kusiguana kwa mapande ya miamba juu ya mipasuko ya ardhi ya bonde hilo la ufa.
Katika siku za karibuni kumekuwepo na taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii ikiwemo facebook, Twitter, Blogs, Instagram na Makundi mbalimbali ya Whatsup jambo ambalo lilinilazimu kufunga safari na kuweka kambi ya takribani siku nne Mkoani Kagera ili kubaini ukweli wa namna fedha zilizopatikana na zilivyotumika ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine jinsi yalivyopatikana na namna yalivyoelekezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...