THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HAKI ELIMU YAISHAURI SERIKALI KUHARAKISHA UUNDAJI WA BODI YA KITAALAMU YA WALIMU

Na Anthony John,Globu ya Jamii

Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na Elimu nchini, HAKI ELIMU limeishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.

Ushauri huo,umekuja baada mapema mwezi huu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi kutoa waraka Na.5 wa Mwaka huu 2016 unaoleta Mabadiliko kadhaa katika program za Mafunzo ya Ualimu nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa shilika Hilo la HAKI ELIMU, John Kalage amesema miongoni mwa Mabadiliko hayo ni kwenda mamlaka ya usimamizi wa Elimu ngazi ya Cheti na stashahada kutoka NACTE na kuyarudisha wizarani chini ya uangalizi wa baraza la mitihani NECTA.

Kalage amesema kuwa kwamujibu wa waraka huo programu za Mafunzo ya Ualimu zitakuwa Astashahada Cheti, na stashahada , Diploma Mafunzo taraji ya stashahada ya juu ya Elimu sekondari yalikuwa yakitolewa kuanzia Mwaka wa masomo 2014/15 yamesitishwa.

"Wizara ya Elimu ndio itakuwa ikitoa maelezo ya sifa za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu, Necta itakuwa inasimamia Mafunzo ya Ualimu huku ikitahini na kutoa tuzo", amesema Kalega.
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John Kalage katikati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.Kulia ni Meneja Habari na Utetezi-Haki Elimu,Elisante Kitulo,Kutoka Kushoto ni Maneja Udhibiti Ubora Haki Elimu,Robert Mihayo.