KOCHA Mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri amesema ameajindaa vizuri ‘kuikabili’ Young Africans kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliopangwa kuchezwa kesho jumatano kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Muda mfupi uliopita Kocha Phiri ameiambia mbeyacityfc.com kuwa anaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kwa sababu timu zote mbili zimetoka kushinda mechi zake zilizopita huku akiahidi ‘kuiduwaza’ Yanga kwa kipigo kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya kwa kikosi chache na kutupilia mbali hofu yoyote kutoka kwa timu hiyo akiamaini timu zote hizi mbili zina mchezo sawa.

“Kweli,kesho tunacheza na Yanga, utakuwa mchezo mzuri kwa sababu timu zote zimeshinda michezo iliyopita,sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda,hatuna shaka yoyote kwa sababu timu zote zina mchezo sawa, jambo jema ni maandalizi tuliyoyafanya na sapoti ambayo tutaipata kutoka kwa mashabiki wetu,watu waje uwanjani na wajiandae kushangaa kile kitakachofanywa na timu yangu”alisema.

Akiendelea zaidi kocha huyo raia wa Malawi alisema kuwa City imebakiza michezo miwili, wa kesho na ule wa tarehe 7 dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Manungu Turiani hivyo anachokitizama sasa ni kushinda michezo hii miwili ili kuweza kupata pointi 6 ambazo zitaicha timu City kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kabla ya kukamilika kwa duru ya kwanza.

“Tumebakiwa na michezo miwili, wa kesho na ule ambao tucheza dhidi ya Mtibwa, tuko kwenye nafasi ya tisa sasa, lengo letu ni kushinda michezo hii ilikuweka mazingira mazuri katika msimamo wa ligi kabla hatujamaliza duru ya kwanza, hii ina maana kuwa tutakapo rejea kuanza duru ya pili tutacheza kwa nguvu kutafuta nafasi mbili za juu” alimaliza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...