THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HIFADHI YA TAIFA YA MSITU WA MKWENI UPO HATARINI KUTOWEKA KUTOKANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Na Evelyn Mkokoi

Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Ukwemi uliyopo katika wilaya ya Kahama upo hatarini kutoweka kutokana na shughili za kibinadamu zinazofanywa ndani ya hifadhi hiyo zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Hayo yameelezwa na Meneja kutoka wakala wa Taifa wa Misitu Bw. Mohamed Dosa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea HIfadhi hiyo iliyopo ndani ya Halmashauri ya Kahama inayopakana na Halmashauri ya Mbongwe Mmkoani geita.

Katika Ziara yake ya Ukaguzi wa Mazingira katika Hifadhi ya Msitu Huo, Naibu Waziri Mpina alielezwa kuwa shughuli kubwa zinazotegemewa na wakazi wa vijiji vya jirani na msitu huo ni, ukataji miti kwa uchomaji wa mikaa na ukataji wa magogo kwa shunghuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na shughuli na ujenzi na utengenezaji wa samani za majumbani.

Meneja Dosa Amemuelezea Naiubu Waziri Mpina kuwa (generation) kizazi cha kwanza cha aina na miti ndani ya hifadhi hiyo kilishakwisha na miti inayoota na kuonekana sasa ni ya kizazi cha pili.

“changamoto kubwa tunayokumbana nayo katika kulinda hifadhi hii ni magari ya doria kuzunguka ndani ya msitu kwani ni mkubwa sana na hakuna skari wa kutosha kufanya doria. “ Alisisitiza Bw. Dosa.

Akiwa katikati ya Msitu huo Naibu Waziri Mpina alijionea Uharibifu mkubwa wa uchomaji mkaa na kushuhudia mhalifu Bw John Abdalah Sanga makazi wa kijiji cha jirani cha mwendakulima aliyekuwa akimaliza kuchoma mkaa katikati ya msitu huo na kueleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa takribani miaka mitatu sasa hali iliyompelekea Naibu Waziri Mpina na timu yake kutekekeza baadhi ya matanuru ya mkaa ndani yam situ huo.

Kwa upande wake Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa Bw. Jamal Baruti alieleza kuwa hali ya uharibifu wa misitu nchini bado ni kubwa na suala la mkaa bado ni changamoto, hivyo wanaanchi washiriki katika kuhifadhi misitu na kutafuta mbadala wa mkaa na misitu ni muhimu kwa kutunza baiyonuwai., wakati katibu tawala wa wilaya ya kahama Bw. Thomas Nganya akitoa Rai kwa wananchi waone kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na siyo kuiachia seriali peke yake. 
Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Mkwemu iliyoharibiwa vibaya na shughuli za binadamu ikiwa na pamoja na uchomaji wa mkaa, na baadhi ni magogo yanayoonekana pichani yaliyokuwa yamekatwa na wahalifu wa mazingira.
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika kuteketeza tanuru la mkaaa katikati ya hifadhi ya m situ ya Mkwemu Wilayani Kahama.
Aliyeshika kiuno, Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiangalia Tanuru la Mkaa likitekea baada ya kushiriki kuteketeza ndani ya Msitu wa Mkwemu wilayani Kahama. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    wananchi wa vijijini wengi hutumia mkaa kulingana na hali yao ya maisha kwani mkaa umekuwa ni bei rahisi kulinganisha na bei ya gas.

    Hivyo ni vyema wawasaidie kupunguza bei ya gas ili kila mwananchi hata wa hali ya chini aweze mudu kununua ili matumizi ya mikaa yaondoke.