Baada ya kuachia video/wimbo wake wa kwanza ‘NOMA’ miezi michache iliyopita, msanii Coyo ambaye ni mwenyeji wa jiji la miamba, Mwanza anatambulisha kazi yake mpya NJOO BAADAE, ikiwa ni ya pili kuachiwa akiwa chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment. 
Akizungumzia wimbo wake mpya, Coyo anasema, “NJOO BAADAE ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila siku ya vijana”.
“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe zako ambazo haziendani na stori  zake, hivyo unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae.” Ameongeza. 
NJOO BAADAE imeandikwa na Coyo ambaye pia amefanya viitikio vya kuimba, na muziki wake umeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi wa Tetemesha Ent.
                                                             
Wimbo wa NJOO BAADAE pamoja na Instrumental vimeambatanishwa hapa, share na wengine kadri uwezavyo.       
Tazama video yake iliyopita ‘NOMA’ hapa: https://youtu.be/VEPUTJL_Tj8

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...