Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali
(wapilikushoto) akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali
Mstaafu, Mhe. Salum Kijuu pindi alipomtembelea ofisi kwa Mkuu wa Mkoa
huyo kumpa pole kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
mnamo tarehe 10.09.2016 na kusababisha maafa katika baadhi ya
miundombinu mkoani huo, Mahakama Kuu ikiwa mojawapo. Kulia ni Mhe.
SalvatoryBongole, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Kanda ya Bukoba.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, (wa
pili kulia) akikagua jengo la Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba ambalo
lilipata mipasuko ‘minor cracks’ kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea
mkoani Kagera. Pamoja ni Jaji Kiongozi, wa pili kushoto ni Mhe. Jaji
Matogoro, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, wa nne kushoto ni
Mhe. Ilvin Mugeta, Msajili- Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye
aliambatana na Mhe. Jaji Kiongozi katika ziara yake Mkoani humo.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Salvatory Bongole,
akiongea kitu mbele ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Bukoba kabla
ya kumkaribisha rasmi Mhe. Jaji Kiongozi kuongea na Watumishi wa
Mahakama wa Kanda hiyo mara baada ya kukagua jengo la Mahakama
lililopata maafa kufuatia tetemeko la ardhi.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Salvatory Bongole,
akiongea kitu mbele ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Bukoba kabla
ya kumkaribisha rasmi Mhe. Jaji Kiongozi kuongea na Watumishi wa
Mahakama wa Kanda hiyo mara baada ya kukagua jengo la Mahakama
lililopata mipasuko kufuatia tetemeko la ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...